Mmmmh I wish ningemwona Magufuli Nipige magoti Nimpongeze hadharani
Yaani Rais wa muungano wa Jamhuri Mchapakazi hachoki Anaye pinga nani?
Mmmh, Ametuvusha vikwazo Wewe nami ona nchi anavyoijenga Flyover sa tunazo, daraja kigamboni Airport imesha jengwa
Acha nikupongeze Kwa Air Tanzania (Ielewe) Zidi baba tuongeze Airbus Bombardier (Ielewe) Standard gauge tuteleze Kusafiri unasinzia (Ielewe) Acheni tu niwaeleze Magufuli papa nia (Ielewe)
Sekta ya madini Umeme maji kero zimepungua (Asa wee) Elimu bure vijijini Watoto shule wanabukua (Asa wee) Ifikapo elfu mbili na ishirini Kura yangu chukua (Asa wee) Asa tufiche ya nini ‘Magu’ uongozi anaujua (Asa wee)
Dar es Salaam mwendo kasi Vituo vya afya kila kata (Ielewe) Machinga tunachapa kazi Tena huru bila shaka (Ielewe) Borigi utani ameongeza Uchumi uweze panda (Ielewe) Serekali Dodoma inapendeza Tanzania ya viwanda (Ielewe)