Eti mziki shetani, pesa nazo shetani Mpira na pombe shetani Mademu na mihadarati, shetani
Naamini Mungu yupo najua Ndo ananifanya ninapumua Akitaka hata sasa ananichukua Ila mi nataka kujua
Ni nini dunia Dunia dunia dunia Hivi ni nini dunia Dunia eeh
Mmmh wanaoishi kwa imani Misikitini makanisani Uwepo wao hauonekani Hali zao zipo taabani
Hivi ulikuaga wapi before Hujaja duniani Na kwanini kunakifo Unapokwenda hapajulikani
Sawa safari ni yetu sote Na hakuna aliyekwenda na akarudi Japo kutusimulia Kama pazuri ama pabaya
Uwe tajiri ama masikini Kwa mchanga utarudi
Minatoa wosia tusiishi kwa ubaya Kunakidude kinaitwa mapenzi Hakijawahi kueleweka Wakati wewe unalia mwenzako yeye anacheka
Hivi ni nini dunia dunia dunia Ni nini dunia, dunia eeh Eeh Pedezye Kumbuka Msalimia mwijaku
Tuombeane mwisho mwema (eeh eeh yeah) Tuombeane mwisho mwema (maana hakuna anaejua kesho) Tuombeane mwisho mwema (kama wewe muislamu) Tuombeane mwisho mwema (omba kwa dini yako) Tuombeane mwisho mwema (kama wewe ni mkristo) Tuombeane mwisho mwema (nisiri nisiri) Tuombeane mwisho mwema (tuombeane nisiri) H