Nimeamini ya leo sio ya jana (Kweli ya leo sio…) Vizuri kufa na ujana Ila life ya Dunia ni tamu sana
Hizo sekunde na dakika Bora ningerudi nyuma Niwe bonge la bitozi Hata salamu ningeuchuna
Mbio zimegonga ukuta Kusanuka kisha nuka Na matuta nimeruka nimeanguka Siwezi tena nyanyuka
Ata ata shabaa Alinitonya wewe ni rafiki Bar Nikapuuza kwa kujawa na mzaa wa kitaa Ghetto la dastamina pia nikalikataa Nilihisi kama nabanwa (kweli nilitoswa…)
Wewe niliyekulea ukiumia nafeel pain Mtetezi juu yako kama jeshi la UN Ulidaiwa sikusita kukulipia madeni Leo iweje uniingize mkengeni
Nimeamini apangalo mola Huwezi pangua yeye ndiye anayejua Ningejua jinsi alivyo kuwa Nisingejisumbua kumchukua
Nilikuwa ndani ya ghetto Na settle mipango ya kesho Mara ring ring, kucheki alikuwa mwana Story ilikuwa hivi nanukuu michapo
Mwanangu sio siri unazari la mentally Kuna binti mtaa wa pili anadai anakukubali Anasema nyimbo zako unajua panga mistari Tajiri hatari wacha tuchume mali
Isitoshe anafiga matata hana dosari Leo leo ukienda atakuhonga hata gari Kifupi sijajivunga na pozi zilikimbia Ulofa nilionao mnyamwezi nikajitupia Upendo kasi kama goli la First
Tuliishi kwenye bangalo Sio nyumba za guest Shida nilishinda hata kwa manji navimba Kumbe nimepewa goma limepigwa sindimba Yule dada ni muathirika nilitumika bila kinga Na mchizi alishajua na potimba nachinjwa
Hee, hee, heee Heee heee hee Nimeamini apangalo mola Hawezi pangua yeye ndiye naejua Ningejua jinsi alivyo kuwa Nisingejisumbua kumchukua