Eeh Mmmh mmh Hivi kwanini nijitutumue Na dunia sio makazi Vijineno neno vinisumbue Hadi nishindwe kazi Mama alisema mkuku kwa nguruwe Kuishi na watu kazi Achambe atukane ata aniue Nishasamehe mzani ni mzazi
Mwenzenu naficha naficha Mengi nayoyaona Kifupi nafunika kombe Nikiamini kesho nayo siku Mapicha picha mapicha Sidhani kama nitapona Wanangu wa mtaani mniombee Hii vita ni mchana na usiku Oooh kuna watu na viatu Wanatamani milele wawe wao Ukijituma watasema Unashinda nao
Oooh ni kama watu kumbe Ndani wana roho za chatu Hawatosheki na vikubwa vyao Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao Mola nipe ujasiri Kwenye kufanya maamuzi Zidi nikomaza akili Isinipoteze miluzi Uniamshe alfajiri Kama jana na juzi Kupata kukosa ni siri Nawe ndo Mungu baba mwamuzi
Dear Lord, wapo Iyeiye iye, wapo Japo ni ngumu kuwaona, wapo Wapo wasotaka ufanikiwe Binadamu hawana jeru, wapo Kila utachofanya watasema, wapo Wapo wasotaka ubarikiwe Dear Lord mmh
Watakuita mwanga kibonge Tena kwa dharau wakucheke Wanachotaka we uongee Waseme shukrani ya punda mateke Kama vipi dem wake tumgongee Ndiye anayempiga chura teke Usipoonewa ndonge Basi ndo ujue hauna makeke Sikia Konde kwepa bana mjini shule Ukipata kidogo leta na nao tule Wachana nao wamesemaga umezoea vya bure Maana siku zote nyani halioni kundule
Kama baba na mama ndo nguzo ya dunia Wapende wote Sio wa kike anacheka wa kiume analialia Bila msaada wowote
Oooh kuna watu na viatu Wanatamani milele wawe wao Ukijituma watasema Unashinda nao Oooh ni kama watu kumbe Ndani wana roho za chatu Hawatosheki na vikubwa vyao Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao Mola nipe ujasiri Kwenye kufanya maamuzi Zidi nikomaza akili Isinipoteze miluzi
Uniamshe alfajiri Kama jana na juzi Kupata kukosa ni siri Nawe ndo Mungu baba mwamuzi Dear Lord, wapo Iyeiye iye, wapo Japo ni ngumu kuwaona, wapo Wapo wasotaka ufanikiwe Binadamu hawana jeru, wapo Kila utachofanya watasema, wapo Wapo wasotaka ubarikiwe Dear Lord
“Special message to the Youth” It’s your time now to follow your dreams No matter what people say stay humble Stay positive, follow your dream Believe in God, ease your mind Ease your mind for Lord (The Most Wanted Mix)