B boy, mm Oh-wah, ah, oh-wah Oh-wah, ah, oh-wah Oh-woah-woah-oh
Alisema mapenzi vita Mi na yeye tuungane kuwateketeza maadui, eh, maadui Badala ya miezi kupita, aah Vikombe lazima vigongane Na sio kwamba hayajui, eh, hayajui
Pigo za kusema vya ndani mi sinaga hizo Ama kumtafuta mchawi ni nani ni kuongeza tatizo Tulia hapa tutakuwa wa ndani hadi paradiso Na tukatangaza kweupe mambo hadharani Na tattoo ndo hizo, oh-oh-oh-oh-oh
Sitaki kuamini kwamba Lile kapu la mabaya yangu Halina hata machache mema, oh, mema Nitakuwa mshamba Nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu Ili nionekane mwema
Japo mapenzi yanaumiza I wish tusisemane (vibaya) oh-le-le-le (vibaya) Ili kesho tusizikane (vibaya) oh-no-no (vibaya) Usiwasikilize wapambe (vibaya) Wanachotaka maneno (vibaya) ili kesho watuchambe (vibaya) oh-oh-oh-oh (vibaya)
Nitunzie siri zangu Nami nitunze zako za miaka rudi nenda Kuna leo na kesho, mm-mm-mm Hata maadui zangu walikuwaga maadui zako Hawawezi kukupenda Wanakuvuta uwe kichekesho, mm-mm
Maana hata ukisambaza Picha zangu za aibu ni sawa Hata hunikomoi Na hata utupu wako ukiutandaza Kwa watu wangu wa karibu sio dawa, hujengi hubomoi, eh-eh-eh-eh-eh
Mama kuna kamchezo Mtunze mtoto wako Na watu wenye majungu, majungu Nilikubali kuviacha vya dezo Sababu ya mapenzi yako Nikaachana na mzungu, mzungu
Maneno yao utadhani wanakutetea Kumbe tudhalilishane wanachongojea Usiwape faida wambea Na ni kama kawaida nakuombea