Imagine uko jangwani umepotea Mchana juani unatembea Utokapo ni mbali uendapo ni mbali Mara ngamia mbebaji akatokea Na kukushusha mzigo uliokuelemea Upate afadhali pole na safari And thats why today To me yote tisa ila kumi Umeonesha maana ya upendo Si kwa maneno bali kwa vitendo Umeridhika na nilichonacho Vya watu hutoleagi macho Siku nikiwa sina twalala Oooh baby twalala Aaaah baby if I close my eyes Mi namuomba Mungu akulinde Na akusimamie we ndo Pacha wangu mie
Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena Sikusikii ukilia sikusikii ukisema Niko busy na boo jamani nimeshasema Niko busy na baby na msalaba wake
Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba Na ntafika nao kiume Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha) Nitaubeba (ama kwenye shibe na njaa) La kwako ndo langu my darling Na ntafika nao kiume
Imagine hujifahamu Umezimia umewekewa damu zinaingia Bomba ikafunguka na huwezi hata nyanyuka Mara dakitari wa zamu Akaingia umepata fahamu unamwangalia Machozi yanakuanguka unatamani funguka And that’s why today to me Yote tisa ila kumi unanifurahisha Kwenye tendo Au unipe penzi la magendo Aaaah baby if I close my eyes Mi namuomba Mungu akulinde Na akusimamie we ndo pacha wangu mie
Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena Sikusikii ukilia sikusikii ukisema Niko busy na boo jamani nimeshasema Niko busy na baby na msalaba wake
Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba Na ntafika nao kiume Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha) Ntaubeba (ama kwenye shibe na njaa) La kwako ndo langu my darling Na ntafika nao kiume
Iwe kwenye shida na raha Ama kwenye shibe na njaa La kwako ndo langu my darling